Habari

ARSENAL HII SASA AIBU!!! YAPIGWA TENA 5-1 NA BAYERN MUNICH …yaaga Champions League kwa karamu ya 10-2

on

Baada ya kufungwa 5-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bayern Munich,
Arsenal imekubali kichapo kingine kikubwa cha 5-1 kutoka kwa miamba hiyo ya
Ujerumani.
Kwa matokeo hayo, Arsenal imeaga Champions League kwa jumla ya magoli 10-2.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Arsenal walikuwa wa kwanza
kupata bao kunako dakika ya 20 kupitia kwa Theo Walcott na kudumu hadi
mapumziko.
Dakika ya 53 sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny akalambwa kadi
nyekundu iliyofuatiwa na penalti iliyozaa goli la kusawazisha mfungaji akiwa
Robert Lewandowski.
Bayern ikafunga tena kupitia kwa Arjen Robben dakika ya 68, Douglas
Costa dakika ya 78 huku  Arturo Vidal akahitimisha
karamu ya magoli kwa kutupia wavuni michomo miwili dakika ya 80 na 85.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *