AZAM FC WAMPELEKA JOHN BOCCO AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI YA GOTI

NAHODHA wa Azam FC, John Bocco amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu ya goti la mguu wa kulia.

Bocco aliumia Januari 28, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya samba, siku ambayo alifunga bao pekee  timu yake ikishinda 1-0 uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi, Bocco yuko Afrika Kusini akifanyiwa matibabu ya goti hilo.


“Alianza kufanyiwa matibabu hapa nyumbani baada ya kuumia, lakini bahati mbaya imekuwa ikichukua muda kupona, hivyo uongozi umeona bora akatibiwe huko,” alisema.

No comments