BAFETIMBI GOMIS ATEGWA KWA PAUNI MIL 18 NA KLABU YA NICE UFARANSA

KLABU ya Nice ya Ufaransa sasa iko tayari kuweka mezani kitita cha pauni mil 18 kwa ajili ya kumnasa straika wa Olympique Marseille, Bafetimbi Gomis, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports.

Straika huyo raia wa Ufaransa ameingia katika rada za Nice inayopambana kwa ajili ya kuweka heshima katika Ligi ya nchini kwake.

Wakitambua hilo, Nice wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni mil 18 wakiongeza dau waliloweka awali ambalo lilikuwa ni pauni mil 15.

Nice walimthaminisha Mfaransa huyo kuwa ni wa dau la mil 18 ingawa wameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.

Marseille pamoja na kuweka bayana thamani ya mchezaji huyo, imethibitisha pia kuwa straika huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu mbalimbali za Ulaya.

“Bafetimbi anawindwa na timu nyingi za Ulaya lakini nataka acheze katika kikosi ambacho atapata namba ya kudumu.”


“Ni mchezaji mwenye ofa nyingi lakini ni jambo la kusubiri kuona ifikapo mwisho wa kipindi cha usajili,” ilieleza tovuti ya klabu ya Marseille.

No comments