BANKY W ASAINI MKATABA MPYA NA KAMPUNI YA SUMSUNG

MWANAMUZIKI Banky W amesaini mkataba mpya na kampuni ya teknorojia ya Samsung ambayo imekuwa ikimdhamini.

Msanii huyo amesaini mkataba huo ikiwa ni wiki chache tangu nyumba yake ilipoungua moto na kupoteza mali zake.

“Imekuwa ni heshima kubwa kufanya kazi na kushirikiana na kampuni hii ya samsung. Pongezi kwa meneja Emmanouil Revmatas na timu nzima,” alisema Banky.

“Nimefurahishwa na kazi tulizofanya hadi sasa, nafurahishwa na changamoto ambazo tutazikabili tukiwa pamoja.”


Tukio la nyumba yake kuungua lilitokea Februari 28, mwaka huu lakini ilielezwa kuwa hakukuwa na mtu aliyepoteza maisha.

No comments