Habari

BASTIAN SCHWEINSTEIGER BYE BYE MANCHESTER UNITED

on

Kiungo aliyekuwa anasugua
benchi Manchester United Bastian Schweinsteiger amekamilisha mpango wa kujiunga
na Chicago Fire ya Marekani.
Inaaminka dili hilo lilikamilika Jumatatu usiku ingawa nyota huyo wa Kijerumani bado hajakamilisha vipimo vya pamoja na kupata ‘visa’.
“Siku zote katika maisha yangu ya soka, nimekuwa nikihitaji kuwa sehemu nitakayosaidia kujenga jambo lenye mafanikio,” ameeleza Schweinsteiger.
“Safari yangu ya kujiunga na Chicago Fire haina tofauti. Nimeshawishika na mipango ya klabu na nataka kuwasaidia kufikia malengo.”
Inatajwa kuwa Schweinsteiger amesaini mkataba wa mwaka mmoja utakaomwingizia pauni milioni 3.6 mwaka 2017, dili litakalomfanya awe miongoni mwa wachezaji 10 wanaolipwa zaidi katika ligi ya Marekani (MLS).

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *