BEKI WA BOURNEMOUTH AMSAFISHA IBRAHIMOVIC KIWIKO ALICHOMPIGA

BEKI wa timu ya Bournemouth, Tyrone Mings amesema kuwa hana uhakika kama kiwiko alichopigwa na straika wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic alikuwa amedhamiria.

Kauli ya beki huyo imekuja baada ya juzi Zlatan kumpiga kiwiko katika mchezo ambao Manchester United walikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Bournemouth wakiwa nyumbani katika michuano ya Ligi Kuu England.

Tukio hilo limekuja baada ya Mings kumshutumu Ibrahimovic kabla ya mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Hata hivyo, akizungumza juzi mara baada ya mechi hiyo, Mings alisema kwamba anavyodhani straika huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Sweden hakudhamiria kumpiga kiwiko, lakini akasema alifurahia kwa jinsi walivyokuwa wakipambana.

“Sioni kama alikuwa amedhamiria kwani haya yalikuwa ni mapambano ya soka, sioni kama kuna shida,” alieleza staa huyo kupitia katika taarifa aliyoituma katika tovuti ya klabu.


“Yalikuwa ni mapambano mazuri ambayo kila mmoja aliyafurahia,” aliongeza staa huyo kabla ya kusema kuwa anavyodhani msimu huu amefanya kazi nzuri kama ilivyo kwa mabeki wote wa Ligi Kuu na huku akiahidi kuendelea kufanya hivyo hadi atakapostaafu.

No comments