BIFU LA DIAMOND PLATNUMZ, ALI KIBA LAMCHEFUA "BABU TUPOGO"... awataka kujirekebisha kwa kuwa "ni ndugu"

HALI ya kuwekeana bifu baina ya Diamond Plutnumz na Ali Kiba inaonekana kuwachefua wengi akiwemo mkongwe wa Domo la Bata, King Maluu "Babu Tupogo"anayewataka wasanii hao kujirekebisha.

Akiongea jana katika kipindi cha Afro Tz cha radio One Stereo kinachoendeshwa na mtangazaji Rajab Zomboko, King Maluu alisema kuwa anasikitika kuona hali hiyo ikijitokeza kwa wasanii hao aliowaita ndugu kwa vile wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma.

“Mi najua kuwa bifu lao linakuzwa zaidi na mashabiki, lakini ni vyema na wao wenyewe wakatafakari na kuangalia umuhimu wao kwa jamii kama kioo, hata enzi zetu bifu zilikuwepo lakini ziliishia kwenye kazi tu,” amesema.


Ametoa mfano wa magwiji wawili wa muziki wa dansi nchini Kongo (DRC), Tabu Rey na Franco ambao pamoja na kuwa na uhasimu mkubwa wa kimuziki, lakini waliwahi kutengeneza albamu moja ambayo inaendelea kutikisa hadi leo.

No comments