BONDIA DAVID HAYE ADUNDWA KWA "KO" NA TONY BELLEW

HATIMAYE bondia David Haye ameushangaza ulimwengu wa mchezo huo baada ya kujikuta akipoteza pambano lake dhidi ya Tony Bellew.

Kabla ya kupanda ulingoni, Haye ndie aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea lakini alishindwa kuvuka raundi ya 11 ya pambano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa 02 Arena, ulioko jijini London, England.

Awali, Haye alisema alifikia uamuzi wa kudundana na Bellew kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa ngumi.

Haye aliingia ulingoni juzi kwa mara ya pili tangu aliporejea mwaka jana ikiwa ni baada ya kujiweka kando ya mchezo huo kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.

Ikumbukwe kuwa Bellew mwenye umri wa miaka 34, alitwaa ubingwa wa Dunia wa WBC mwaka uliopita baada ya kumdunda Ilunga Makabu katika pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Goodison Park.


Hata hivyo kabla ya pambano hilo la juzi, Bellew alifikiri wazi kuwa alichukua uamuzi wa kijasiri kutwangana na bingwa huyo wa zamani wa Dunia.

No comments