BONDIA FATUMA ZARIKA AKISHUKIA CHAMA CHA NGUMI CHA WBC AKIDAI NI MATAPELI

BONDIA mahiri kutoka nchini Kenya, Fatuma Zarika amesema kuwa chama cha ngumi cha WBC ni miongoni mwa matapeli wanaopaswa kuchunguzwa na FBI.

Fatuma ambaye mwaka jana alijiandikia rekodi ya kuwa bondia wa kwanza mwanamke kutoka Afrika Mashariki kushinda taji la dunia la ndondi za kulipwa, amesema hadi sasa hajalipwa.

Bondia huyo aliyemtoa nishai Alicia Ashley wa Jamaica katika pambano lililofanyika nchini Marekani akitwaa ubingwa wa Dunia uzani wa super-bantam, aliahidiwa kutumiwa fedha zake.

“Ninashangaa kwa nini FBI wasiwachunguze WBC, ni matapeli wakubwa, waliahidi kunitumia fedha zangu za ubingwa wa Dunia mwaka jana, lakini nashangaa mpaka sasa sijalipwa,” alisema Fatuma.


Bondia huyo aliiambia BBC kwamba alipata taarifa kutoka kwa mabondia wengine kuwa imekuwa kawaida ya vyama vingi vya ngumi duniani kuwanyanyasa mabondia wanaotoka nje ya Marekani. 

No comments