BONDIA STEPHEN THEGA AKUMBWA NA MATATIZO YA UBONGO

BONDIA wa zamani aliyepata kuvuma akiwa na timu ya taifa ya Kenya, Stephen Thega amekubwa na matatizo ya akili.

Tegha alivuma sana katika miaka ya 1970 akiiwakilisha Kenya katika ndondi ambapo aliwahi kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 1972.

Taarifa zilizothibitishwa na familia yake zinasema kuwa hivi sasa bondia huyo anaugua maradhi ya ubongo na huenda akapelekwa nchini Marekani kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 


Familia yake inasema kuwa inajaribu kuwasiliana na wizara ya michezo na marafiki zake, ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya matibabu hayo.

No comments