BOSI WA VIJANA JAZZ BAND AJIFAGILIA KUMFUNDISHA MUZIKI JESICA CHARLES

KIONGOZI wa Vijana Jazz Band, Sabuli Athuman ameibuka na kumtaja aliyewahi kuwa mwimbaji mahiri wa kike ndani ya Twanga pepeta, Jesica Charles kuwa miongoni mwa wasanii ambao wamepitia kwenye mikono yake katika kuwafundisha muziki.

Akipiga stori na Saluti5 hivi karibuni, Sabuli alisema kuwa alikutana na Jesica kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma akiwa bado hajaanza muziki na wakati huo akiishi kwa mama yake mdogo.

“Kwa kuwa alikuwa anapenda muziki na alionyesha kuwa na kipaji nilianza kumfundisha na hakuchukua muda akawa anamudu kuimba bila wasiwasi na hapo safari yake rasmi ya muziki ikaanza rasmi,” alisema Sabuli.


Alisema, mbali ya Jesica wapo pia wasanii mbalimbali aliowanoa na ambao hivi sasa wanatesa kwenye muziki Bongo.

No comments