BOSI WA ZAMANI WA PATORANKING MATATANI KWA UNYANYASAJI KWA MKEWE

BOSI wa zamani wa mwanamuziki Patoranking, Fuston amehusishwa na vitendo vya unyanyasaji kwa mkewe.
Hayo yameibuliwa na mkewe aitwaye Ajoke ambaye amedai kuwa Fuston alikuwa akimtesa ikiwemo kumtembezea kichapo mbele ya marafiki zake.

Baada ya mama huyo kuweka mambo hadharani, watu wa karibu wa lebo inayomilikiwa na Fuston iliyowahi kusimamia kazi za Patoranking, wamethibitisha ukweli wa taarifa hizo.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kabla ya kuoana, lakini mara kadhaa Ajoke alikuwa akipigwa kiasi kwamba hakukaukiwa majeraha mwilini.

Mbaya zaidi, Ajoke amedai kuwa alikuwa akipigwa mara 20 kwa kipindi cha mwaka mmoja na mwanaume huyo na alijaribu kumuua mara tatu.


“Hakuwa na huruma na mara nyingi alisema anataka kunitoa damu. Alifunga milango yote hata maeneo ambayo ningeweza kutokea,” alisema.

No comments