CANNAVARO AWAAHIDI WANA YANGA KUPAMBANA HADI DAKIKA ZA MWISHO

WACHEZAJI wa Yanga wamezisikia sana tambo za watani wao Simba, Lakini wakajibu kwa kusema hawatakubali kuuachia ubingwa kwa maneno bali watapambana hadi dakika ya mwisho.

Akizungumza na Saluti5 wiki iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” aliwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwaunga mkono.

Alisema, pamoja na tambo za Simba lakini hadi hivi sasa wao wanaamini ndio watakaoutetea ubingwa wao ambao wameushikilia kwa misimu miwili  mfululizo.

Cannavaro alisema, kama wanachama watawapa sapoti ya kutosha haoni kitakachowazuia kutetea taji lao na kulinyakua moja kwa moja kutokana na kanuni za sasa za mashindano hayo.


Mpaka hivi sasa nafasi ya ubingwa wa msimu uu umebaki kwa Yanga na watani zao Simba wakati timu nyingine zimebaki kupigania kulinda heshima lakini sio ubinwa wa kuwa zimeachwa kwa pointi nyingi huku Ligi ikielekea ukingoni.

No comments