CHARLZ BABA AVAMIA JUKWAA LA MSONDO NGOMA NA KUPAGAWISHA MASHABIKI JUMAMOSI

CHARLZ Baba “Kingunge” amedhihirisha kuwa ana uwezo wa kufanya kazi popote na maisha yakaendelea kama kawaida, baada ya Jumamosi kuvamia jukwaa la Msondo Ngoma na kupagawisha mashabiki.

Tukio hilo lililovuta hisia za mashabiki wengi lilitokea ndani ya Kisuma Inn, Mbagala Sabasaba ambako Msondo Ngoma humwaga burudani kila wiki.

Charlz aliyefika ukumbini hapo kutembea, alionekana ghafla akivamia jukwaa na kuimba kibao “Solemba” ambapo mashabiki walianza kumiminika kati kucheza nae huku wengine wakimwogesha noti.

Baadae tena alipanda tena jukwaani kwa nyakati tofauti na kuimba vibao  “Tuma” na “Mwana Mkiwa”. 
 Charlz Baba (kushoto), akiimba sambamba na Juma Katundu
 Hapa Charlz akiendelea kupagawisha
 Utamu wa wimbo umenoga zaidi
 Kazi hapa imenoga zaidi
Hapa Charlz akiwa mezani na wadau baada kumaliza kuimba

No comments