CHELSEA YAIVAA MANCHESTER UNITED VITA YA KUWANIA SAINI YA MLINZI WA AS ROMA

MATAJIRI wa darajani chini ya kocha Antonio Conte wameingia katika vita ya usajili na Manchester United.

Klabu hizo zote za premier zinamwania mlinzi wa klabu ya AS Roma ya Italia, Antonio Rudiger.

Chelsea tayari wameweka mezani dau la pauni mil 35 kwa ajili ya kupata saini ya beki huyo ambae kwa sasa yupo katika kiwango kizuri. 
Kocha  Antonio Conte anamtambua vizuri Rudiger tangu alipokuwa akifundisha ndani ya Ligi seria A.

Mlinzi huyo raia wa Ujermani, mwenye umri wa miaka 24 anatakiwa na klabu Hispania, zikiwemo Atlatico Madrid na Real Madrid.

Rudiger ambae ni mlinzi tegemeo katika kikosi cha taifa Ujermani, aliumia kifundo cha mguu lakini hata hivyo Chelsea wa mesema watamvumilia mpaka apone na kuendelea na mazungumzo ya kumsajili katika dilisha la Januari.

Kocha Conte amethibitisha kumwania Rudiger baada ya kutokamilika kwa mpango wa kuwawania Leonldo Bonucci na Kalidou Koulibaly ambao walikuwa wakiwawinda katika usajili wa majira ya kiangazi.

No comments