CHRISTIAN BELLA AMMWAGIA SIFA DOGO RAMA KWA UIMBAJI

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi Bongo, Christian Bella amemmwagia sifa mwimbaji mwenzie wa miondoko hiyo, Dogo Rama akisema ana kipaji cha aina yake.

Bella amesema Dogo Rama ana uwezo mkubwa ndio maana anaweza kuimba nyimbo za wanamuziki mbalimbali na kuzipatia kwa kiwango cha juu.

Staa huyo alimfagilia Dogo Rama baada ya kuona video iliyotupiwa kwenye ukurasa wake wa facebook ikimuonyesha chipukizi huyo akiimba moja ya nyimbo za Christian Bella.

Video hiyo inamwonyesha Dogo Rama akiwa kwenye moja ya shoo zake ambapo aliimba wimbo huo wa Bella kwa ufasaha.

“Kwa kweli ukiangalia hii video ya Dogo Rama, kama hajatajwa mwimbaji utasema ni mimi, kijana anao uwezo mkubwa wa kukopi kazi achiliambali kuimba nyimbo zake mwenyewe ,” alimfagilia.


Sehemu ya kipande alichoimba Dogo Rama kilisikika “Dogo Rama live in Bella Christian ‘Obama’ nyimbo zote naimba, sina muda wa kuchagua nyimbo sasa hivi…”

No comments