Habari

CHRISTIAN BELLA AMPA TANO DOGO RAMA

on

Mwimbaji supastaa wa dansi Christian Bella amempigia saluti mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta Dogo Rama kwa uwezo wake wa kugandamizia (copy) nyimbo za wasanii wengine.

Hatua hiyo imekuja baada ya Dogo Rama kutupia video kwenye ukurasa wake wa facebook akiimba moja ya nyimbo za Christian Bella.
Video hiyo ilimuonyesha Dogo Rama akiwa kwenye moja ya show zake ambapo aliimba wimbo huo wa Bella kwa ufasaha.
Katika kupost video hiyo Dogo Rama alisindikiza na meneno yafuatayo: “Dogo Rama live in Bella Christian Obama nyimbo zote naimba sinamuda wakuchaguwa nyimbo sasa hivi.”
Dogo Rama alikuwa akimaanisha kuwa yuko jukwaani atatumbuiza kupitia wimbo wa Christian Bella na kwamba sasa hivi yuko fiti kukandamizia nyimbo zote zozote zile.
Miongoni mwa wasomaji wake waliompongeza kupitia video hiyo ni Christian Bella ambaye aliandika hivi: “Umetisha sana kipaji ya juu sio kila mtu anaweza haya mambo”.
Dogo Rama naye akamjibu: “Pamoja jembe unajua sana, wewe ni jamaa yangu sana halafu nakukubali sana Christian Bella”.

Saluti5 inawapongeza waimbaji hawa kwa kupeana sapoti na kupongezana hadharani, kitu ambacho kimekuwa adimu kwa wasanii wa dansi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *