DANIELLA OKEKE WA NOLLYWOOD AKUMBWA NA KASHFA YA KUTEMBEA NA MCHUNGAJI WA KANISA

MWIGIZAJI mahiri wa kike wa Nollywood, Daniella Okeke ametumbukia kwenye kashfa ya kutembea na mchungaji wa kanisa moja maarufu, Omega Fireman, Apostle Johnson Suleman.

Hayo yamefichuliwa na msanii Stephanie Otobo ambaye alimtuhumu mrembo huyo kukosa aibu na kufikia kutembea na mchungaji huyo mpenda uroda.

Otobo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kufichua mambo hayo mazito ambayo yalisababisha Daniella kuzifunga akaunti zake zote za mitandao ya kijamii kujaribu kukwepa aibu kutoka kwa mashabiki wake na watu wengine.

No comments