DAVIDO ALIKOROGA KWA DEMU WA KIMAREKANI

MSANII anayefanya vizuri kwenye soko la muziki barani Afrika, Davido amejikuta akiingia kwenye utata baada ya kutajwa kuwa na mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Tatizo ni kwamba hivi karibuni mwanamuziki huyo alitangaza hadharani kuwa anatarajia kupata mtoto wa tatu na wa kwanza kwa mpenzi wake aitwaye Amanda anayeishi Atlanta, Marekani.

Hivyo ni wazi kuwa taarifa za kuwa na mtoto mwingine wa kike anayetajwa kwa jina la Veronica zinaweza kumsababishia matatizo kwa demu wake huyo.

Hata hivyo, wawakilishi wa Davido hawajazungumzia chochote kuhusu madai hayo.


Davido mwenye utajiri unaotajwa kufikia dola za Kimarekani mil. 14.5 na mrembo wake huyo wanatarajia kupata mtoto wa kiume Aprili au Mei, mwaka huu.  

No comments