DEFOE NYOTA YAMWAKIA UZEENI …AREJESHWA KIKOSI CHA ENGLAND


Mshambuliaji mkongwe wa Sunderland Jermain Defoe, 34 ameitwa kwenye kikosi cha England ikiwa mara ya kwanza tangu alipotumikia nchi yake mwaka 2013.

Kocha wa England Gareth Southgate amemjumuisha Defoe kwenye kikosi hicho kinachojiandaa kukabiliana na Germany na Lithuania.

Katika michezo huyo ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia, Southgate pia amewaita kwa mara ya kwanza Nathan Redmond na James Ward-Prowse.

No comments