DEMETRIA DEVONNE ASHEREHEKEA MIAKA MITANO YA MAFANIKIO KAMA MWANAHARAKATI

MWIGIZAJI mwanamuziki na mwanaharakati wa watu wasiojiweza Demetria Devonne maarufu kama “Demi Lovato” amesherehekea kutimiza miaka mitano ndani ya harakati na akawashukuru mashabiki kwa kumfikisha hapo.

Demi aliandika katika mtandao wake wa kijamii kwamba alijitosa rasmi kwenye sanaa na kufahamika kikazi Machi 15, 2012.

“Ni faraja isiyo kifani kupata mafanikio haya ndani ya miaka mitano, lakini sdikupata haya kwa akili na ujanja wangu bali ni mapenzi ya Mungu na nawashukuru wazazi na mashabiki wangu,” alisema.


Alisema hakutarajia kupata mafanikio aliyonayo ndani ya muda mfupi lakini lakini yote yamewezekana kutokana na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa mashabiki wake.

No comments