DENTI ALIYEMPORA DRAKE MKOBA WENYE DHAHABU NA FEDHA ATUPWA JELA MIAKA SITA

YULE mwanafunzi mtukutu, Travion King aliyempora Drake dhahabu yenye thamani ya dola mil 3, fedha taslim na vito vingine, amepigwa mvua sita.

Katika shitaka la kwanza la kukiri kutenda uhalifu, Travion King amehukumiwa kutumikia jela mwaka mmoja katika gereza la Maricopa Country Jail.

Baada ya kumaliza adhabu hiyo, atatumikia miaka mingine mitano kamili katika gereza lingine na jaji amesisitiza, ili iwe fundisho, ni lazima King atomize miaka yote gerezani.

Mwanafunzi huyo aliyelazimika kuachana na ndoto za masomo, alimkaba Drake Septemba mwaka jana wakati raia huyo akijiandaa kutumbuiza mjini Phoenix na kumpora mkoba wake uliokuwa na dhahabu, fedha taslim na vito vya thamani.


Katika utetezi wake, King ambaye alinaswa na polisi akiwa na baadhi ya vitu hivyo shuleni, alikiri kuiba na kujitetea kwamba alitaka apate fedha za kumwezesha kupata mpenzi wa kizungu.

No comments