DOMINIC SOLANKE ANUKIA LIVERPOOL BAADA YA CHELSEA KUMRUHUSU KUSEPA

PENGINE windo la timu ya Liverpool kwa kiungo kinda wa Chelsea, Dominic Solanke likafanikiwa kiangazi cha mwaka huu.

Liverpool iliyokuwa ikimfukuzia Solanke mwenye umri wa miaka 19 kwa muda, sasa inaweza kumpata bure baada ya kuruhusiwa kuondoka baada ya yosso huyo kutaka mshahara mkubwa wa pauni 50,000 kwa wiki.


Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema anamruhusu kwa roho nyeupe kinda huyo kuondoka Stanford Bridge kwani hayuko tayari kumlipa kiasi hicho cha fedha.

No comments