DONALD NGOMA, AMISSI TAMBWE KUONGEZEWA MKATABA MPYA YANGA

UVUMI wa kuondoka kwa mshambuliaji Donald Ngoma umezimwa rasmi baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kuwaongezea mkataba mpya pamoja na Amissi Tambwe. 

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinasema tayari uongozi wa juu umeshapata baraka zote kutoka kwa benchi la ufundi waliopendekeza kuongezewa mikataba kwa washambuliaji hao.

Bosi mmoja anayesimamia usajili amesema wakati wowote kutoka sasa washambuliaji hao wataingia katika mazungumzo ya kuongeza mikataba hiyo ambapo mbali na hayo, pia ataongezwa mshambuliaji mmoja.

Lengo la kuongezwa mshambuliaji huyo mpya ni katika kuwaongezea ushindani washambuliaji waliopo sasa huku pia ikiwa ni akili ya kukabiliana na upungufu wa washambuliaji endapo kutakuwa na majeruhi kama ilivyo sasa.

“Tunawaongezea mikataba mipya Tambwe na Ngoma, tayari benchi la ufundi limeshatupa ruhusa la kuendelea katika kuanza nao mazungumzo,” alisema bosi huyo.


“Tumeambiwa katika kumuongezea mkataba Ngoma, lakini pia tutafute mshambuliaji mwenye asili kama yake na mwenye uwezo zaidi ili aweze kuwapa changamoto hawa wa sasa.

No comments