DORTMUND WAJIPA MATUMAINI YA AUBAMEYANG KUENDELEA KUBAKI NAO

MKURUGENZI mtendaji wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amesema ana uhakika staa wao, Pierre-Emerick Aubameyang atabaki kwenye klabu hiyo ya Signal Iduna Park ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Kwa sasa straika huyo mkali ana mkataba na BVB hadi juni 2020, lakini kumekuweko na habari zinazomuhusisha kuondoka kwenye kikosi hicho cha Ligi ya Bundesliga huku Real Madrid ikitajwa kummezea mate.

Hivi karibuni pia ziliibuka tetesi zinazodai Aubameyang anaweza kuondoka ili aweze kupiga hatua nyingine katika kibarua chake, lakini majuzi Dortmund wakasema kuwa wana uhakika ataendelea kuwatumikia.

“Tangu kipindi ambacho auba alipojiunga na Dortmund hajawahi kuwa na mawazo ya kuondoka ndani ya klabu hii,” Watzke aliliambia jarida la Bild.


“Na ninavyodhani tumejenga timu kali na ninadhani tunafahamu kile anachotufanyia na vilevile na sisi tunafahamu tunachoweza kufanya tukiwa nae,” aliongeza kigogo huyo.

No comments