DULLAH MAKABILA ASEMA HAKUFIKIRIA KAMA KIBAO "MAKABILA" KINGEMPANDISHA ZAIDI

DULLAH Makabila ambaye ni msanii wa mziki wa singeli ambaye anayekuja juu kwa sasa amefichua kwamba hakuwahi kufikiria kama kibao chake cha “Makabila”kingeweza kuchukua chati kiasi cha kumfanya awe maarufu hapa Bongo.

Akiongea na Saluti5 msanii huyo ambaye sasa anatamba na kibao kingine kipya kinachokwenda kwa jina la “Hujaulamba”, amesema kwamba anashukuru kuona kibao hicho kimemtoa kwenye maisha ya kuwa tayari hata kupiga shoo za sh. 5,000.

“Wakati natunga kibao hiki sikua na mawazo kwamba kitakuja kufanya vizuri nakunipandisha chati kama livyo hivi sasa ambapo nimeachana na maisha magumu ya kisanii niliyokuwa nikiishi huko nyuma,” alisema.


Alisema kuwa kazi iliyobaki kwake hivi sasa kuhakikisha anatoa wimbo mpya kila baada ya muda mfupi ili kuepuka kusahaulika ama kupotea kwa kipindi kirefu masikioni mwa mashabiki anaoamini kwamba ndio mabosi zake.

No comments