EDDO SANGA APATA AHUENI… aanza kutembea umbali mfupi bila kutumia magongo


MWIMBAJI mahiri wa Msondo Music Band, Eddo Sanga amepata nafuu ya miguu iliyokuwa ikimsumbua kwa takriban miezi miwili sasa.

Saluti5 imemtembelea Eddo nyumbani kwake leo mchana na kupiga nae stori mbili tatu ambapo amethibitisha kuwa hivi sasa anamudu kutembea kwa kuchechemea umbali usio mrefu.

“Ni tofauti na nilivyokuwa hapo awali, sasa hivi situmii magongo kwenye kutembea ingawaje bado nachechemea kwa mbali,” amesema Eddo ambaye ni kati ya watunzi wenye uwezo mkubwa katika dansi kwa sasa.


Eddo alianza kusumbuliwa mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu kwa miguu kuwa mizito na kushika ganzi kidogo kidogo kuanzia nyayoni hadi sehemu za tumboni, kabla ya baadae kupoteza kabisa uwezo wa kukanyaga na kutembea.

No comments