FM ACADEMIA WALIPOPATA BARAKA ZA RAIS MSTAAFU MH. JAKAYA KIKWETE


Bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” jana jioni ilipata kismet cha kukutana uso kwa uso na rais mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Kikwete.

Wasanii wa bendi hiyo walikuwa wakichukua picha za video maeneo ya Michokechi jijini Dar es Salaam jirani  na nyumbani kwa JK.

Kwa bahati nzuri rais mstaafu alipokuwa akirejea nyumbani kwake, aliwaona wasanii wa FM Academia na kuwasalimia na ndipo wanamuziki  hao kwa heshima na taadhima wakaomba fursa ya kupiga stori mbili tatu pamoja na wasaa wa kupiga picha za kumbukumbu na kiongozi huyo kipenzi cha watu.

Rais mstaafu hakuwa na hiyana, akawakaribisha nyumbani na kuwapa fursa ya kubadilishana mawazo kwa dakika kadhaa, kabla wasanii hao hawajotoka na kuendelea na shughuli ya kupiga video ya nyimbo zao mpya.
 Nyoshi el Saadat (kushoto) akiwa na rais mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Kikwete
Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani kwa wasanii wa FM kupata wasaa wa kupiga picha  na rais mstaafu  Mheshimiwa Jakaya Kikwete

No comments