FUNUNU ZA LEONARDO BONUCCI KUTAKA KUSEPA CHELSEA ZAITESA JUVENTUS

HABARI zinazozidi kusambaa kwa kasi kwamba beki wa kati wa Juventus ya Italia, Leonardo Bonucci anajiandaa kuhama Chelsea, zimeitesa zaidi klabu yake hiyo ya sasa.

Juzi viongozi wa Juventus wanadaiwa kumbana na kumuuliza beki huyo kama ni kweli kinachoandikwa kwenye mitandao na magazeti makubwa ni sahihi.

Hata hivyo, beki huyo katili anadaiwa kukataa kujibu chochote akisema kwamba angependa amalize mkataba wake kwanza ndipo aseme mengine.

Beki huyo wa kati amedaiwa kwamba hana mahusiano mema na kocha wake wa sasa katika Juventus, Massimiliano Allegri na kwamba ameshatangaza muda mrefu kwamba atahama kama kocha huyo atakuwa ndio kiongozi wa kikosi hicho.

Habari hizo ndizo ambazo zimedaiwa kumsisimua kocha wa Chelsea ambaye pia ni raia wa Italia, Antonio Conte ambaye amekuwa akisema siku zote kuwa Bonucci ni mmoja wa mabeki wagumu duniani kwa sasa.

Manchester City yenyewe ilijaribu kumsajili Leonardo Bonucci msimu uliopita lakini ikashindwa na wakaishia kumsajili John Stones.


Lakini hata hivyo miamba hao wa Italia wamedaiwa kuanza kujiandaa na uhamisho huo na ndio maana wamekuwa wakiwategemea sana George Chellini na Andrea Barzagli.

No comments