G5 MODERN TAARAB KUINGIA STUDIO WIKI IJAYO KUPAKUA NONDO TATU KALI


Kundi la miondoko ya muziki wa mwambao G5 Modern Taarab, wiki ijayo litaingia studio kurekodi nyimbo tatu mpya.

Mmoja wa viongozi waandamizi wa G5 Omar Kisila ameiambia Saluti5 kuwa kundi hilo litarekodi nyimbo hizo katika studio za Sound Crafters zilizoko Temeke jijini Dar es Salaam.

Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni “Safari Yangu Salama”, “Kikomo cha Mnafiki” na “Nimepata Nusura”.

“Safari Yangu Salama” utaimbwa na Kibibi Yahaya huku “Kikomo cha Mnafiki” mwimbaji atakuwa  Aisha Masanja. Nyimbo zote mbili zimetungwa na Captain Temba na muziki umepangwa na Omar Kisila.

“Nimepata Nusura” utaimbwa na Fadhila Mnoga, mdogo wake na mwimbaji nyota wa dansi Hadija Kimobitel. Wimbo huu umetungwa na kutiwa muziki na Omar Kisila ambaye pia ni mmoja wa wakali wa kupapasa kinanda hapa nchini.
Kibibi Yahaya anakuja na  “Safari Yangu Salama”
“Kikomo cha Mnafiki” na  Aisha Masanja
Fadhila Mnoga anashuka na “Nimepata Nusura”


No comments