GARETH BALE ALIMWA RED CARD YA KWANZA TANGU 2008 HUKU REAL MADRID IKILAZIMISHA SARE ...BARCELONA YAUA 6-1


Gareth Bale jana alilimwa kadi nyekundu ya kwanza tangu aanze kuitumikia Real Madrid katika mchezo wa La Liga ulioisha kwa sare ya 3-3 dhidi ya Las Palmas kwenye dimba la Santiago Bernabeu. 

Hiyo inakuwa red card ya kwanza kwa Bale tangu Oktoba 2008 wakati akiichezea Tottenham dhidi ya Stoke City. 

Isco aliifungia Real Madrid bao la kuongoza dakika ya nane, bao lililodumu kwa dakika mbili tu kabla ya Tana Dominguez hajaisawazishia Las Palmas kwa shuti kali lililomshinda kipa  Keylor Navas.

Dakika tatu baada ya mapumziko Gareth Bale akatolewa baada ya kuzawadiwa kadi mbili za njano za papo kwa papo.

Kuanzia hapo jahazi la Real Madrid likayumba na kupelekea Jonathan Viera kuifungia  Las Palmas  bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 56 kabla  ya Kevin-Prince Boateng hajaongeza goli la tatu dakika tatu baadae.

Cristiano Ronaldo akafunga haraka haraka dakika ya 86 na 88 na kuipa sare Real Madrid.

Wakati Real Madrid ikibanwa kwa sare, mabingwa watetezi Barcelona wakaendelea kucharuka kwa kuilamba Sporting Gijon 6-1 ambapo Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wote walifunga mara moja kila mmoja.

No comments