Habari

GARETH BALE ATAKIWA KUSALIA SANTIAGO BERNABEU HADI MWAKA 2026

on

SASA ni
dhahiri kuwa kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale hawezi kuondoka katika miaka ya
hivi karibuni ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.
Hii ni baada
ya kuwepo kwa mazungumzo mapya ya kutaka awe mchezaji wa kudumu licha ya
kandarasi yake ya sasa kuonyesha itafika tamati ifikapo mwaka 2022.
Raia huyo wa
Wales sasa amejifunga pingu kwa miaka sita hadi mwishoni mwa mwaka 2022, lakini
kocha wake Zinedine Zidane ameomba Bale awe na mkataba mrefu zaidi ikiwezekana
hadi mwaka 2026.
Bale mwenye
umri wa miaka 28, alitua Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham Hotspur kwa
dau lililovunja rekodi wakati ule, la pauni mil 86.

Taarifa za
ndani ya klabu hiyo ya jiji la Madrid zimebainisha kuwepo kwa mazungumzo
yanayoendelea hivi sasa ya kutaka kiungo huyo amalize maisha yake ya soka ndani
ya Madrid.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *