SIKIA HII... ETI MSANII GENEVIEVE NNAJI AFUNGA NDOA YA SIRI!

KUNA uvumi kuwa supastaa wa kike tajiri ndani ya Nollywood, Genevieve Nnaji amefunga ndoa ya siri hivi karibuni.

Wadaku wamesema ndoa hiyo imefungwa katika kisiwa kimoja nchini Ufaransa ingawa mwenyewe msanii huyo ameshindwa kukanusha wala kuthibitisha taarifa hizo.


Mwaka jana Nnaji na mchumba wake Ogochukwu Udezue walikorofishana dakika za mwisho kabla ya kufunga ndoa mjini Milan nchini Italia ambapo bwana alitaka wafanye sherehe kubwa lakini bi harusi mtarajiwa akasisitiza iwe siri na hilo likawa sababu ya kuachana.

No comments