Habari

GILBERTO SILVA ASEMA SASA WENGER ANAPASWA KUTIMKA ARSENAL

on

Mmoja wa nyota wa Arsenal iliyomaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja (Invincibles), amekiri kuwa sasa umefika muda wa  Arsene Wenger kuachana na klabu hiyo.
Gilberto Silva ambaye msimu wa 2003-04 alikuwa mmoja wa mashujaa wa Arsenal iliyoweka rekodi ya kipekee Premier League, anasema Wenger anazidiwa maarifa na wapinzani wake vijana Antonio Conte, Pep Guardiola na Jurgen Klopp ambao wameziimarisha vilabu vyao.
Wenger yupo kwenye shinikizo kubwa kutokana na tishio la timu yake kumaliza nje ya Top Four kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996 huku mkataba wa kocha huyo Mfaransa ukiisha mwishoni mwa msimu huu.
“Nadhani huu ni muda muafaka wa yeye kuondoka”, kiungo huyo wa Kibrazil aliiambia Sport 360.
“Kadri siku zinavyosonga ndiyo anavyopaswa kuondoka – sio kwasababu hajui kazi, ila labda ni kwasababu timu zingine zimebadilisha mfumo wao wa kufanya kazi.
“Hajabadilika, mfumo wake ni ule ule, sio kwasababu hataki ila ni kwasababu ni ngumu kuchuana na timu zinazomwaga pesa nyingi kila msimu”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *