GRIEZMANN AIPOTEZEA MAN UNITED… asema akiondoka Atletico hatakwenda United, PSG, China, Marekani wala Urusi wanakomwaga fedha

MSHAMBULIAJI anayefukuziwa sana na arsenal na Manchester United, Antoine Griezmann, amezitolea nje timu hizo.

Griezmann amesema kuwa ni kweli anajiandaa kuondoka Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu lakini ni iwapo tu atapata ofa kutoka kwa Barcelona, Real Madrid au Bayern Munich.


Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 25, amesisitiza kuwa akiondoka Atletico hatakwenda popote, iwe United, PSG, China, Marekani ama Urusi wanakomwaga fedha, bali atakwenda kwenye timu itakayompa mataji na heshima barani Ulaya.

No comments