GUARDIOLA AKANA KUTOA AHADI YA MATAJI MANCHESTER CITY... asema waandishi walimnukuu vibaya

PEP Guardiola ameibuka na kudai kuwa hakuahidi kuchukua mataji alipotua Manchester City.

Guardiola amedai vyombo vya habari vilimnukuu vibaya wakati anatua Etihad kwani hakusema kuwa ataipa timu hiyo ubingwa.

“Mimi ni kocha, nawajibika kwa kila kilichotokea (dhidi ya Monaco), alisema Guardiola.

“(Waandishi) hamko sahihi. Sikuja hapa na kusema tutashinda.  Sikusema tutashinda mataji matatu, sikusema nitachukua ubingwa mara mbili. Sikusema.”

Kauli ya Mhispania huyo imetokana na kitendo cha timu yake kufungwa na Monaco na kuondoshwa kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Guardiola aliongeza kuwa ugumu ulioko kwa timu yake unatokana na matarajio makubwa yanayotegemewa kutoka kwake.

Taarifa zilizopo ni kwamba Guardiola  amepanga kufanya marekebisho makubwa kwenye kikosi chake ambapo atatumia pauni mil 200 kusajili sura mpya.


Imeelezwa kuwa huenda panga likawafyeka Vincent Kompany, Bacary Sagna, Gael Clichy, Pablo Zabaleta na mastaa wengine walioshindwa kung’ara Etihad.

No comments