GUARDIOLA AKIRI KIBARUA KIGUMU MANCHESTER CITY

KOCHA Pep Guardiola amekiri akisema kwamba changamoto anazozipata akiwa na kikosi cha Manchester City ni tofauti na alichowahi kukabiliana nacho wakati akizinoa timu za Bayern Munich na Barcelona.

Wiki iliyopita Manchester City ilitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Monaco kwa faida ya bao la ugenini ikiwa ni mara ya kwanza kwa Guardiola kushindwa kufika walau hatua ya nusu fainali tangu aanze kufundisha soka.

Huku kwa sasa vinara wa Ligi Kuu, Chelsea wakiwa mbele yao kwa tofauti ya pointi 13 dhidi ya kikosi cha wawakilishi wake hao katika michuano ya Kombe la FA wanaoonekana kuwa na nafasi moja ya kumpa ubingwa wa kwanza katika msimu wake wa kwanza nchini England, wakati Man City watakapoikabiri Arsenal katika hatua ya nne bora mwezi ujao.

Kutokana na hali hiyo, kiungo huyo wa zamani wa Barca anasema kwamba bado anatakiwa kufanya mipango mbalimbali ili kutengeneza timu ambayo anaitaka kama alizofundisha nyuma na akasema kuwa anavyoamini itamchukua muda hadi kuyafikia mafanikio yake ya nyuma akiwa na klabu hiyo ya Etihad.

“Itanichukua muda kutengeneza timu ambayo naitaka,” kocha huyo aliiambia Sky Sports News.

“Kwa klabu nyingine, kwa sababu nyingine nyingi kuna ushindani wa karibu. Kwa hapa itachukua muda,” aliongeza.


Alisema kuwa hata hivyo jambo hilo ndilo analolihitaji kutokana na kuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na hali hiyo na akasema kuwa kwa upande mwingine ni bahati kwake kama kocha.

No comments