HAJI MANARA ASEMA “HII SIO SIMBA NINAYOIJUA” …adai timu ilicheza soka mbovu


Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara, amesema klabu yake ilimwangusha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City siku ya Jumamosi.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ililazimika kusawazisha kila wakati ili kuambulia sare ya 2-2.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji ameandika: “Sio Simba nnayoijua mimi, tumecheza soka hovyo mno , but we will make it”.
No comments