HARRY KANE AJIFAGILIA "MUBASHARA"… asema anaamini yeye ni miongoni mwa wachezaji bora duniani

STRAIKA wa Tottenham, Harry Kane ni kama anajipa ujiko baada ya kusema anavyoamini yeye ni miongoni mwa wachezaji bora duniani kutokana na kuwa ndie anayeongoza kwenye msimamo wa wafungaji bora katika michuano ya Ligi Kuu England.

Hadi sasa Kane ameshafunga mabao 17 msimu huu sawa na mastraika Romelu Lukaku na Alexis Sanchez na huku msimu uliopita akiwa ameshatwaa kiatu cha dhahabu.

Staa huyo wa timu ya taifa ya England mwenye umri wa miaka 23, alikwea kileleni mwa msimu huo baada ya kuvunja rekodi ya kupiga “hat-trick” wakati wa mechi yao ya Jumapili ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City na sasa anavyodhani anajiamini kwa uwezo wake.

“Endapo utaangalia uchezaji wangu na mabao yangu, nadhani nipo katika daraja hilo,” alisema Kane ambaye msimu huu ameshafunga mabao 22 katika mashindano yote.


“Endapo utataka kuliandika hilo nitakuwa na furaha kubwa na nitajaribu kujituma kutokana na kuwa napenda kufunga mabao, kwa ujumla nitajaribu kufunga kadri niwezavyo kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu kutokana na kuwa najihisi nipo kwenye ubora,” aliongeza staa huyo.

No comments