HASSAN SALUM KABUNDA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU KWA MWEZI FEBRUARI

KIUNGO mshambuliaji wa Mwadui FC, Hassan Salum Kabunda ndie mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari mwaka huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba Kabunda amewapiku washambuliaji wa Simba, Raudit Mavugo na Ibrahim Ajibu baada ya mechi tatu za Februari kushinda tuzo hiyo.

“Kabunda amecheza dakika 270 katika mechi tatu ambazo Mwadui wameshinda mbili na kupoteza mechi moja hivyo kujikusanyia pointi sita na kupanda kutoka nafasi ya nane hadi ya sita,” amesema Lucas.  

Aidha, Ofisa Habari huyo wa TFF amesema motto huyo wa beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa “Taifa Stars” Salum Kabunda enzi zake akiitwa “Ninja” au “Msudan”.


Katika mechi hizo tatu alifunga mabao manne kati ya sita ambayo Mwadui ilifunga na kwa ushindi huo Kabunda atazawadiwa sh. mil 1 na wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom.

No comments