HATIMAYE AFRICAN LYON YAWEKWA SOKONI... gharama kubwa za uendeshaji bila uzalisahaji wa kutosha yatajwa kuwa sababu

IMEBAINIKA kuwa timu ya African Lyon ambayo imerejea Ligi Kuu Tanzania Bara imewekwa sokoni akitafutwa mnunuzi mwenye mkwanja wa kutosha.

Ingawa mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangenzi “Zamunda” amekanusha kuiuza akisema wanataka kuimarisha uwekezaji, lakini ukweli ni kuwa anaipiga bei timu hiyo.

Imeelezwa kuwa gharama kubwa za kuendesha timu bila ya kuwa na uzalisahaji wa kutosha ndio unaomsukuma kuiuza timu hiyo.

Kwa sasa mazungumzo baina ya African Lyon na kampuni ya GSM Limited yanaelekea kukamilika.


African Lyon iliuzwa mwaka 2010 na mfanyabiashara anayetaka kumiliki hisa nyingi ndani ya Simba SC, Mohammed Dewji “Mo”, ambaye pia aliinunua mwaka 2007 kutoka kwa wafanyabiashara wa soko la Mbagala, wakati huo ikiitwa “Mbagala Market”. 

No comments