HATIMAYE SASA MAJI YAMFIKA SHINGONI ARSENE WENGER... akiri anaweza kusepa muda wowote

KOCHA  Arsene Wenger ameifundisha klabu ya arsenal kwa miaka 21, lakini wiki hii ameweka hatma yake ya miaka ijayo katika wasiwasi kuliko wakati mwingine wowote katika uongozi wake.

Kubanduliwa kwa mara ya saba katika hatua ya 16 bora katika Ligi ya mabingwa Ulaya ulikuwa uchungu wa kutosha bila kuongeza pigo la magoli 10-2 kutoka kwa Bayern Munich.

Malalamiko dhidi ya Wenger yamekuwa yakisikika chini kwa chini kwa miaka mingi lakini sasa malalamiko hayo yameongezeka.

Kwa mwaka huu wote mkataba mpya bado uko mezani huku meneja huyo mwenye umri wa miaka 67 akisema maoni ya mashabiki yatachochea uamuzi wake iwapo atasalia kama meneja.

Wenger kila mara hukosolewa na vyombo vya habari na mashabiki wengi wamezoea kupata habari na mabadiliko na sio uthabiti wake.

Alisema maneno sawa na hayo yeye mwenyewe.

Liverpool hawajawahi kushinda Ligi ya Uingereza na Manchester United wamechukua muda tangu kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini wawili hao wamekuwa na zaidi ya mameneja mmoja mmoja.

Akizungumza na Daily Mail, Wenger amesema kwamba kwa sasa bado hajajua hatma yake, lakini kelele za mashabiki zikizidi anaweza kuangalia namna ya kumalizana na uongozi wake.

“Bado sina cha kuzungumza kwa sasa kuhusu hatma yangu, lakini kama kelele zikizidi, sina la ziada maana itanilazimu tu kukaa pembeni,” amesema Wenger.


Na hii ni mara ya kwa Wenger kukiri hadharani kwamba kibarua chake kwa sasa kipo shakani kwani mara zote husema kuwa hafikirii kuondoka ndani ya timu hiyo hivi karibuni.

No comments