JACK WOLPER AWATAKA WATANZANIA WASIMCHARURE MAKONDA "ISHU" YA KUFOJI VYETI

NYOTA wa kike wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amemkingia kifua mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwataka watu kuacha kumwandama kwa kashfa yake ya kufoji vyeti pamoja na kumtukana mitandaoni.

Kwa wiki kadhaa sasa Makonda amekuwa akisakamwa mitandaoni kutokana na tuhuma kuwa jina analotumia si lake na kwamba lake ni Daudi Bashite.

Jumapili hii kumesambaa video mitandaoni ikimuonyesha mkuu huyo wa mkoa akilia kwa uchungu kanisani baada ya kuzungumza na mchungaji akimbembeleza.

“Nimevaa kiatu chake kimenibana mpaka kinataka kunipasua kisigino,” ameandika Wolper kwenye Instagram.
“Jamani Watanzania tuwe na utu, acheni kumtukana huyu kaka daaah, hivi ni nani ambaye yuko perfect mpaka aanze kumtukana kaka wa watu jamani.”


“Nimeposti nikiwa kama binaadamu wa kawaida ambaye nina moyo, mhurumieni kaka wa watu, acheni Mungu awe mhukumu basi,” aliongeza.

No comments