JAHAZI YANYOFOA MWIMBAJI MMOJA WA MASHAUZI CLASSIC


Bendi mbili za taarab zinazoaminika kuwa ni ndugu, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic, zimeendelea kuimarisha ‘undugu’ wao kwa msanii mmoja kutoka kundi moja kwenda lingine.

Mwimbaji chipukizi wa Mashauzi Classic Mariam Kasola (pichani juu) amejiunga rasmi na Jahazi Modern Taarab na jana kwa mara ya kwanza alikwea jukwaa la bendi hiyo katika onyesho lao lililofanyika Travertine Hotel Magomeni.

Kihistoria Mariam Kasola anakuwa msanii wanne kutoka Mashauzi na kujinga na Jahazi. Wa kwanza alikuwa Rahma Machupa akafuata Emeraa Solo kabla hajafuatia Rajab Kondo.

Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Sumaragar alipoulizwa na Saluti5 juu ya mwimbaji huyo kujiunga na Jahazi akasema riziki popote na hivyo wanamtakia kila la kheri.

“Hakuonekana kazini kwa muda mrefu kwa kuwa alikuwa anaumwa lakini tetesi za kutakiwa kwake na Jahazi tulikuwa nazo muda mrefu na tuliwauliza viongozi wa Jahazi mara kadhaa lakini wakawa wanakanusha. Si jambo baya Jahazi ni ndugu zetu hivyo tunaamini kuwa bado yuko nyumbani. Milango iko wazi kama  wanahitaji msanii mwingine kutoka kwetu, tunaamini bado wanahitaji wengine,” alisema Sumaragar.

Naye boss wa Jahazi Juma Mbizo aliiambia Saluti5 kuwa walikuwa hawajui kama msanii huyo bado alikuwa anaitumikia Mashauzi Classic.

“Alituambia ameacha kazi Mashauzi miezi mingi iliyopita,” alisema Mbizo.

No comments