JE, UNAZIJUA NYIMBO NNE ZA DIAMOND PLATNUMZ ZINAZOMKOSHA WAZIRI KINGWANGALLA? SOMA HAPA!

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta Hamis Kingwangalla ameonekana kuvutiwa na wimbo mpya wa Diamond Platnumz “Marry You” ambao amemshirikisha Ne-Yo kutoka Marekani.

Kiongozi huyo kupitia mtandao wa Twitter amesema kuwa hajawahi kuwa shabiki wa Diamond lakini anazipenda nyimbo nne za mwimbaji huyo, hukua kionekana kuunyooshea mikono wimbo wa “Merry You” ambao mpaka sasa umefanikiwa kutazamwa mara mil 5 kwenye mtandao wa Youtube.


“Sikuwahi kuwa shabiki wa Diamond Platnumz japokuwa ni mwimbaji mzuri, ila nakubali sana kipaji chake kwenye biashara ya muziki. Zaidi ya nyimbo ya Diamond Platnumz “Mbagala” (ambayo naipenda mpaka kesho), na juzi hapa nyimbo ya “Ngololo”, “Salome”, hii ya “Marry You”.

No comments