JOHN BOCCO ASEMA AZAM FC UBINGWA UTAWAHUSU IWAPO WATAIFUNGA YANGA

NAHODHA wa Azam FC, John Bocco amesema wataingia kwenye mbio za kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kama wataifunga Yanga kwenye mchezo wa marudiano.

Azam FC na Yanga zinatarajiwa kurudiana wiki tatu zijazo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bocco amesema, watahakikisha wanaifunga Yanga kwenye mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu msimu huu ili kuwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.

Alisema, watahakikisha wanaifunga Yanga ili kuikimbiza Simba iliyoko kileleni mwa Ligi na wana matumaini ya kupata ushindi kutokana na kikosi chao kuamkana kuanza kufanya vizuri.

Aidha, nahodha huyo alisema kocha wao wa sasa raia wa Romania ni mzuri na anaeleweka kwa wachezaji ukilinganisha na alivyokuwa Zeben Hernandez aliyetimuliwa.


Azam inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 44, pointi tisa nyuma ya Yanga yenye pointi 53, lakini Azam imeachwa kwa pointi 11 na Simba ambao ndio wanaoongoza Ligi hadi sasa baada ya timu hizo tatu kucheza michezo 24 kila moja.

No comments