JOHN TERRY AVAMIWA NA MAJAMBAZI NYUMBANI KWAKE

WEZI wanaaminika kuvunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza, John Terry, wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.

Maafisa wa polisi wa Surrey walithibitisha kwamba nyumba iliyopo Oxshott ilivunjwa wikiendi iliyopita.

Msemaji wa kituo hicho cha polisi cha Surrey amesema kuwa: “Tunaweza kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliyopo Moles Hill, Oxshott, usiku wa tarehe 25 na 26 mwezi Februari.”


Wezi hao wanadaiwa kuvunja na kuingia katika nyumba hiyo na kuiba vitu vyenye thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 36, alikuwa ameenda likizo na watu wa familia akiwemo mkewe Toni kulingana na ripoti za gazeti la The Sun.

No comments