JOSE MOURINHO AFANYA KITU CHA AJABU KWA NEYMAR

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho anatajwa kuzungumza na nyota wa Barcelona, Neymar katika kutaka kujaribu kumshawishi atue Old Trafford.

Mashetani wekundu hao wanajiandaa kukutana na kifungu cha kutolewa Neymar kwa pauni mil 173 na wameridhia kumlipa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mshahara wa pauni 416,000.

Mourinho amekuwa kwenye mikakati ya kuisuka United akilenga kurudisha hadhi ya miamba hiyo baada ya kupoteza mwelekeo kwa miaka kadhaa sasa.


Hata hivyo, wachambuzi wa soka wanasema itakuwa vigumu kwa United kumng’oa mshambuliaji kutoka Barcelona, ikizingatiwa United si mshiriki wa mara kwa mara kwenye Ligi ya mabingwa Ulaya.

No comments