Habari

JOSE MOURINHO AMNG’ANG’ANIA IBRAHIMOVIC ABAKI MANCHESTER UNITED

on

KOCHA wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anamtaka
mshambuliaji wa klabu hiyo, Zlatan Ibrahimovic kusalia katika klabu hiyo kwa
mwaka mwingine mmoja.
Ibrahimovic mwenye miaka 35, alijiunga na Mancnester United
akiwa mchezaji huru kutoka Paris Saint-Germain kwa kipindi cha msimu mmoja huku
akiwa nafasi ya kuongeza mkataba wake.
Raia huyo wa Sweden amefunga magoli 26 katika mechi 38
msimu huu, zikiwemo bao mbili katika ushindi wa Kombe la EFL dhidi ya Southampton.
“Sote tunataka asalie na tunaamini atafanya ivyo kwa msimu
mwingine mmoja’ alisema mkulunzi huyo.
“Bado nafasi yake ndani ya klabu ya Man United ni kubwa,
hivyo tunataka aendelee kubakia ndani ya klabu hiyo kwa kipindi kingine zaidi
na mchango wake umeonekana kuwa muhimu zaidi kwa kikosi chetu.”
Ibrahimovic alibeba Kombe lake la 32 katika kipindi chake
chote cha soka baada ya kufunga bao dakika 87 katika uwanja wa Wembley.
Katika kipindi hicho Manolo Gabiadiani aliifungia Saints
mabao mawili  baada ya Jesse Lingard
kuiweka Red Devils ikiwa inaongoza kwa 2-1.
Mourninho aliongezea:sipendelei kumbembeleza mchezajikutia
saini kandarasi mpya ama kunichezea.

Wakati Zlatan alipoelekea Barcelona kutoka Inter Milan
nahisi vibaya sana lakini iwapo anahitajika mashabiki wanaweza kwenda hadi
mlangoni kwake kupiga kambi usiku kucha.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *