JOSE MOURINHO APONDA SERA ZA USAJILI ZA LOUIS VAN GAAL


Jose Mourinho ameibuka na hoja ya kushutumu sera mbovu za usajili zilizofanywa na kocha wa zamani wa Manchester United  Louis van Gaal.

Mourinho anadai klabu iliuza wachezaji kimakosa na kwamba kamwe yeye asingethubutu kuuza wachezaji kama Angel Di Maria, Javier Hernandez na Danny Welbeck.

"United iliuza wachezaji ambao kamwe nisingethubutu kuwauza, lakini pia ilinunua wachezaji ambao nisingefikiria kuwanunua. Nisingewauza Angel Di Maria, Javier Hernandez na Danny Welbeck," alisema Mourinho.
No comments